Ng'ombe zaidi ya laki moja wamepewa chanjo ya mapele ngozi katika kata zote za Kwimba,chanjo hiyo ilianza tarehe 01/06/2020 na kumalizika tarehe 30/06/2020.Katika zoezi hilo wataalamu wa mifugo wameweza kugundua changamoto za wafugaji ikiwemo kutotibu mifugo yao kwa wakati,wafugaji hao wameshauriwa kutoa taarifa kwa wataalam wa mifugo pindi wanapogundua tatizo kwa mifugo yao.Aidha wafugaji wameshukuru kwa huduma hiyo na wameomba na magonjwa mengine yanayosumbua mifugo yao yadhibitiwe ili kupunguza upotevu wa mifugo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.