Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imetoa kiasi cha Milioni 100 kwa vikundi vya wanawake na vijana hili limefanyika tarehe 17/11/2020.Vikundi vya wanawake vilivyopata mkopo huo usio na riba ni 35 ambavyo vimepatiwa milion 78.5 na vikundi 6 vya vijana ambavyo vimepatiwa milion 21.5
Aidha kabla ya fedha hizo kutolewa kwa vikundi hivyo Maafisa maendeleo wameweza kuwapatia elimu ya ujasiriamali ili wakazitumie fedha hizo kuongeza kipato.Bi Happyness Kaali Afisa Maendeleo amesema fedha hizo zikazarishwe ili marejesho yaweze kufanyika kwa wakati ili vikundi vingine ambavyo havijapata viweze kupata mikopo, vilevile amewashauri wanavikundi kukata bima ya Afya iCHF iliyoboreshwa ili wawe na uhakika na matibabu kwani bila Afya bora ujasiriamali hautafanyika kama walivyokusudia
Pia wajasiriamali hao wamehamasishwa kukata vitambulisho vya mjasiriamali ili wanapopata mikopo hiyo wakafanye biashara bila kusumbuliwa.
Afisa biashara Ndug. Barnabas Yawanga akiwahamasisha wajasiriamali kukata vitambulisho vya mjasiriamali.
Wakiongea na waandishi wajasiriamali hao wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba kwani itawasaidia kukuza biashara na kuboresha maisha kwa ujumla .
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea kutekeleza agizo la Serikali la kutoa asilia 10 ya mapato yake ya ndani kwa kuwakopesha wanawake,vijana na walemavu mikopo isiyo na riba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.