Ikiwa ni utaratibu wa kila halmashauri kutoa mikopo ya asilia kumi ya mapato ya ndani, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba leo tarehe 9,Sept 2022 imekabidhi milioni 170 kwa vikundi 16 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Akikabidhi mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amevitaka vikundi hivyo kwenda kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa siyo kugawana fedha kitu kinachopelekea vikundi vingi kushindwa kurejesha
“fedha hizi siyo zawadi wala siyo hisani, fedha hizi ni mkopo usio na riba hivyo lazima fedha irejeshwe, kafanyeni kazi mlizoandika kwenye mikataba yenu, hakikisheni fedha hizi zinabadirisha hari ya yenu ya uchumi, hakikisheni fedha hizi zinawainua kutoka hatua moja kwenda nyingine” amesema Samizi
Aidha Afisa Maendeleo ya Jamii(W) Bi. Rozalia Magoti akisoma taarifa ya mikopo hiyo amesema Halmashauri inakabidhi milioni 170 kwa vikundi 16 vya vijàna, wanawake na watu wenye ulemavu ikiwa ni mikopo ya robo ya nne ya April- Juni 2021/22.
Miongoni mwa vikundi vilivyopewa mikopo ni kikundi cha wanawake ambao wamekabidhiwa trekta yenye thamani ya milioni 60, na kikundi cha vija wanaojishughulisha na utengenezaji wa samani za ndani wamekabidhiwa vifaa vyenye thamani ya milioni 22.
Wakipokea mikopo hiyo wameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha hizo na wameahidi kwenda kufanya kazi na kuhakikisha wanajiinua kiuchumi kupitia fedha hizo,pia wameahidi kurejesha fedha hizo kwa wakati ili ziwasaidie watu wengine ambao bado hawajapata mikopo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.