Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepanda miti 6600 katika maeneo ya Taasisi na maeneo ya watu binafsi. Akiongea leo tarehe 26 Feb,2022 katika Kilele cha wiki ya usafi na upandaji wa miti Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amesema
" katika siku hizi za usafi mpaka kufikia leo tumepanda miti 6600 na tunaendelea kewahamasisha Wananchi waendelee kupanda miti ili kupambana na mabadiriko ya tabia ya Nchi, vilevile tunawahamasisha Wananchi kuwa swala la usafi siyo wiki hii tu bali ni endelevu kwahiyo tuendelee kutunza mazingira yetu kwa kufanya usafi na kupanda miti"
Aidha katika kuhitimisha wiki hii ya usafi Wananchi wakishirikiana na viongozi wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kwimba.
Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kuitumia jumamos ya mwisho wa mwezi kama siku ya usafi, amesisitiza kuwa wale watakao puuzia jambo hilo na maeneo yao yakikutwa machafu watatozwa faini kwa mujibu wa sheria.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.