Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongera amesema mpaka sasa Mwanza inatosha kuandaa maonyesho ya Sherehe za nanenane Kitaifa amemuomba Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutumia vigezo vyao ili maonyesho ya nanenane kitaifa kwa mwaka 2018 yafanyike katika Mkoa wa Mwanza.
“Mtupe maelekezo ya kufanya na sasa kanda ya ziwa inasubiri na zamu yetu imefika kuandaa maonesho ya sherehe za nanenane Kitaifa.”
Ameyasema hayo wakati akifungua Rasmi Maonyesho ya Sherehe za Wakulima tarehe o4 Agost,2017 katika uwanja wa Nyamhongoro Mkoani Mwanza.
Aidha amesema kuanzia sasa kanda ya ziwa inajipanga kutatua changamoto za miundombinu katika uwanja wa Nyamhongolo.
“ kuelekea maadhimisho ya mwaka 2018 tunaanza mara moja ujenzi wa miundombinu ya kudumu tunapokuja kwenye maonyesho haya mwaka kesho tutakuta uwanja unakiwango kikubwa cha ujenzi na uwekezaji wa miundombinu ya kudumu nayakisasa kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa na wakurugenzi wote wa kanda ya ziwa.”
Mhe. Mongera ameendelea kumpongeza na kumshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka msisitizo mkubwa kwenye viwanda.Amesema kuwa dhana hii ya viwanda haiwezi kukamilika bila ya kuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo na asilimia themanini ya wananchi wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kupitia kilimo cha mazao, ufugaji na uvuvi hivyo wataamu waendelee kuwaamasisha wananchi kujishughulusha na shughuli za kilimo bora ili kufikia uchumi wa kati.
Naye kaimu mkuu wa Wilaya ya Ilemera Mhe. Khadija Nyembo ameishukuru kamati ya Maandalizi ya Sherehe za nanenane kwa kuandaa maonyesho hayo mazuri.Mhe.Nyembo ameyasema hayo wakati akimkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kuongea na wakulima wa kanda ya ziwa.
Pia Ndg Mathayo Mabirika mjasiliamali kutoka katika kikundi cha Mahiga wilayani Kwimba amesema maonyesho ya mwaka huu ni ya kipekee kwani idadi ya washiriki wa sherehe za maonyesho ya nanenane na wananchi wanaokuja kwa ajilili ya kununua bidhaa za wakulima ni wengi ukitofautisha na sherehe za mwaka jana 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bibi Pendo A.Malabeja akisalimiana na Mkulima wa Zao la Mpunga Ndg Mathayo Mabirika katika Banda la Maonyesho ya Kilimo la Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba
Maonyesho ya ya sherehe za wakulima nanenane ni ya tano (05) kwa mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mara,Simiyu Geita, Mwanza,Kagera na Shinyanga kufanyika katika viwanja vya Nyamhongoro Mkoani Mwanza.Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Shrerehe za Wakulima Nanenane Ndg.Beda Chematata.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.