Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga akiwa ameambatana na baadhi ya Wakuu wa Idara wamekagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Sumve kinachotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani na ujenzi wa Kituo cha Afya Isunga kinachojengwa na fedha toka Serikali kuu.
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa fedha za mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya kipya katika kata ya Sumve.
Halmashauri imetenga milioni 300 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kutekeleza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, maabara na kichomea taka, aidha milioni 100 zimeshapelekwa kwaajili ya kujenga jengo la wagonjwa wa nje( OPD ) na ujenzi umefikia hatua ya boma.
Halmashauri inaendelea kupanga mikakati itakayowezesha kituo hicho kupata majengo yote yanayohitajika katika kituo cha Afya.
Aidha viongozi hao wamekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la upasuaji na ukunga na ujenzi wa jengo la kufulia katika kituo cha Afya Isunga ambapo ujenzi umefikia hatua za ukamilishaji
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.