Elimu ya unyunyiziaji viuwadudu na matumizi sahihi ya vinyunyizi imeendelea kutolewa na Balozi wa Pamba Mheshimiwa Aggrey Mwanri ambapo Leo Februari 5,2023 akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga wametoa elimu katika Kijiji cha Bugandando, Ibindo na Bugando.
Viongozi hao wameendelea kusisitiza juu ya matumizi bora ya viuwadudu ikiwa ni pamoja na kuzingatia vipimo sahihi vya sumu au dawa kulingana na kinyunyizi kinachotumika kunyunyizia.
Akiongea na wananchi wa Ibindo na Bugando Bi. Happiness Msanga amewashauri wakulima kuzingatia elimu hiyo Ili iwasaidie kuokoa zao hilo ambalo linashambuliwa na wadudu wa aina tofauti.
Vilevile ameitumia ziara hiyo kuwatangazia wananchi wenye wanafunzi wanaotakiwa kuripoti kidato cha kwanza ambao bado hawajaripoti kuhakikisha kesho wanaripoti shuleni
" tumefungua Shule lakini watoto hawapo, Sasa kabla hatujaanza kufanya msako wa nyumba Kwa nyumba kama unamtoto yuko nyumbani jumatatu aende shule, madarasa yapo na viti vipo wapelekeni wanafunzi shule hata kama hawana sare za shule mtawatafutia huku wakiendelea namasomo" Msanga
Aidha Mkurugenzi huyo amewashauri wananchi kuhakikisha wanatunza akiba ya chakula baada ya kupata mavuno Ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza " niwaombe mtakapoanza kuvuna mkumbuke kutunza akiba ya chakula msiuze chakula chote mkabaki bila akiba"
Katika mafunzo hayo Mheshimiwa Mwanri ameendelea kuwatangazia wananchi kuwa mwezi wa saba kutakuwa na kampeni ya kung'oa maotea yote ya pamba hivyo wananchi wote watatakiwa kung'oa na kuchoma maotea kabla kamati haijapita kukagua zoezi hilo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.