Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amefanya vikao na Watumishi wa Idara ya Elimu wa vijiji vyote vya Kata ya Sumve.Ikiwa ni utaratibu wake wa kupita kijiji kimoja baada ya kingine kuzungumza na watumishi ili kujua hali ya utekelezaji wa kazi na changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika vikao hivyo Watumishi wameelezea changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa Nyumba za watumishi na miundombinu mingine ikiwemo uhaba wa matundu ya vyoo vya wanafunzi kwa baadhi ya Shule na uhaba wa vitabu vya kufundishia na changamoto nyingine za kiutumishi.
Mkurugenzi huyo amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi, nidhamu na upendo, aidha Msanga amewaeleza Watumishi hao kuwa Changamoto zote zitatatuliwa kwa kuzingatia sheria,kanuni na maelekezo ya Serikali vilevile amewataka Walimu hao kuzigeuza baadhi ya changamoto kuwa fulsa ili waweze kujiongezea kipato kama kujishugulisha na Kilimo, kujenga nyumba za kupangisha nashughuli nyingine nyingi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.