Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewashauri watumishi na viongozi wa kuchaguliwa ngazi ya kata kufanya kazi kwa ushirikiano
Ameyasema hayo leo Julai 22,2024 katika vikao vya kamati za maendeleo za kata vilivyofanyika katika kata ya Igongwa, Ng'undi,Nyamilama,Mwakilyambiti na Mwankulwe
" niwashauri mpende kufanya kazi kwa ushirikiano badala ya kutunishiana misuri" Msanga
Amesisitiza kuwa maendeleo ya mahali popote yanaletwa na jamii ya eneo husika hivyo wananchi wahamasishwe kushiriki shughuli za maendeleo
Mkurugenzi huyo amewataka viongozi hao ngazi ya Kata kuacha tabia ya kutumia fedha za Serikali kwani huo ni wizi na atakayebainika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria
" mnapokusanya michango ya maendeleo pelekeni kwenye akaunti za vijiji au kata acheni kukaa na fedha nyumbani na kujikopesha fedha za umma kwanza ni dhambi na niwizi" amesema Msanga
Bi. Msanga ametumia vikao hivyo kuhamasisha suala la elimu huku akiwataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuwa mabalozi kwenye kuhimiza suala la elimu na maadili.
Naye Afisa Uchaguzi ambaye pia ni Afisa Utumishi Ndugu Clavery Reginald ametumia wasaa huo kutoa elimu ya umuhimu wa kujiandikisha na kuboresha taarifa kwenye daftari la mpiga kura.
Viongozi walioshiriki vikao hivyo wamemshukuru Mkurugenzi kwa kuwafikia katika maeneo yao ili kusikiliza na kutatua kero zao
" Mkurugenzi tunakushukuru sana kwa kutufikia maana umeweza kusikia changamoto zetu naamini utakwenda kuzifanyia kazi na sisi maelekezo yako tunakwenda kuyatekeleza" amesema Mheshimiwa Peter Ngasa Diwani Kata ya Ng'undi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.