Mkurugenzi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Emmanuel Seleman Shindika amewapongeza Walimu wa Wilaya ya Kwimba kwa kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa, ameyasema hayo Jana Mei 31,2024 kwenye kikao kilichofanyika Shule ya Sekondari Ngudu
" nimekuja kuongea na wana Kwimba nikiwa na jambo moja kuu la kuhamasisha na kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya, sifa zenu zimetukuka hongereni sana kwa kuongeza ufaulu " amesema Shindika
Mkurugenzi huyo ameutumia Mkutano huo kuwataka walimu wenye madai mbalimbali wapeleke madai hayo kwa Maafisa elimu ili madai yao yapelekwe sehemu husika kwaajili ya kufanyiwa kazi.
Pia amewataka Maafisa elimu kushughulikia changamoto za walimu ikiwa ni pamoja na muundo, kupanda madaraja,pesa za uhamisho na changamoto nyingine ili kuondoa malalamiko.
Aidha amewataka walimu kujiepusha na mikopo yenye riba kubwa (Kausha damu) inayopelekea wengi kushindwa kutimiza majukumu yao, badara yake wameshauliwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha kama kilimo na ujasiriamali.
Shindika amewashauri walimu kuipenda kazi yao na kuridhika na kipato wanachokipata "chanzo kikubwa cha watu kuteseka ni kutotosheka na kipato wanachopata, Mshukuru Mungu kwa kipato hicho ridhika kisha tafuta mradi mwingine wa kuongeza kipato mradi ambao hautaathiri muda wa mwajiri wako"
Walimu walioshiriki kikao hicho wameahidi kwenda kufanyia kazi ushauri na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wote walioshiriki kikao hicho.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.