Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba awataka Wakuu wa Shule na Walimu wakuu kufanya kazi kwa upendo, ushirikiano na uadilifu. Ameyasema haya kwenye kikao cha robo cha Tathmini ya Shughuli za Elimu, ambacho kimefanyika leo tarehe 08, Oktoba 2021 kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu.
Mkurugenzi huyo amewataka Walimu kufanya kazi kulingana na sheria na taratibu za utumishi.
Amewasisitiza Walimu kusimamia miradi inayotekelezwa katika Shule zao kwa uadilifu. Aidha amesema Walimu wanapaswa kuzingatia miongozo katika utoaji wa adhabu kwa Wanafunzi. "Narudia tena tuache kutoa adhabu zisizo na Afya kwa Wanafunzi" amesema Bi. Happiness Msanga
Mkurugenzi huyo amewataka Walimu kuacha ulevi na amewataka walimu wakuu kutoa taarifa za Walimu walevi ili wachukuliwe hatua, amesisitiza kuwa haizuiliwi kunywa pombe lakini pombe hairuhusiwi mda wa kazi kwa watumishi
"wape masikini kilevi wasahau shida zao lakini kilevi hakifai kwa Mfalme asije potosha hukumu" amesema Msanga
Bi. Msanga amewashauri Walimu hao kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika maeneo yao wanayoishi.
Katika kikao hicho ameshiriki Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Mwalimu Martine Nkwabi ambaye amewataka Walimu kufanya kwazi kwa kuzingatia miongozo, aidha amesisitiza uadilifu katika kusimamia miradi inayotekelezwa na amewataka Walimu wanaopewa nafasi za kuwasimamia wengine kuzitendee haki nafasi hizo.
Amewataka walimu wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na Wanafunzi kuacha mara moja tabia hiyo, " ninachokiona tutapata upungufu wa Walimu kwa sababu wengi watafungwa" amesema Nkwabi
Afisa Elimu huyo amesisitiza kuwa heshima ya mtumishi hailetwi na mavazi, vyeti vyenye A nyingi, utanashati au mali ila heshima inaletwa na huduma anayotoa katika jamii.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.