Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea badara yake wafanye kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma.
Ameyasema hayo leo Novemba 10,2023 katika kikao cha watumishi wa makao makuu (HQ) ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba
" tujireshe kwenye utaratibu, Sasa tutaanza kupimana kwa kazi tunayofanya hivyo kila mtu afanye kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni na kila kazi iwe na matokeo chanya" amesema Msanga
Msanga amewasisitiza watumishi kufika kazini kwa wakati unaotakiwa na kuhakikisha kila mtumishi anatulia ofisini kwake ili atimize majukumu yake.
Aidha Mkurugenzi huyo amewasisitiza watumishi kufanya kazi kwa upendo, ushirikiano na umoja " taasis haiwezi kuendelea kama watumishi hatufanyi kazi kwa ushirikiano, tupendane na tufanye kazi kwa timu hapo tutafanikiwa" Msanga
Naye Afisa Utumishi ( W) Bi. Jane Mallongo ameitumia nafasi hiyo kuwaelekeza watumishi kanuni za utumishi wa umma, pia amewasisitiza watumishi kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za utumishi ikiwemo kutoondoka eneo la kazi bila ruhusa, kutofanya kazi kwa mazoea na kupenda kujiendeleza kimasomo ili kuendana na wakati.
Watumishi walioshiriki kikao hicho wamewapongeza viongozi kwa kuandaa kikao hicho kwani kimewakumbusha mambo mengi yanayohusu utumishi wa umma.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.