Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amezindua maadhimisho ya mwezi wa Afya na Lishe ya mtoto katika Kituo cha Afya Ngumo. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 18, Julai 2022.
Akizindua maadhimisho hayo Bi. Happiness Amewataka wazazi kuhakikisha wananyonyesha watoto wao kwa miezi sita bila kuwapa chakula kingine chochote, amesisitiza kuwa mtoto hapaswi kupewa vyakula tofauti na maziwa mpaka anapofikia miezi sita na kuendelea.
Mwezi wa Afya na lishe huadhimishwa kila mwaka mwezi wa sita na mwezi wa 12 kwa Watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka mitano, huduma hizi hutolewa pamoja na huduma zingine za kawaida za afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Wilayani.Huduma zinazotolewa ni matone ya vitamini A,upimaji wa hali ya lishe ya mtoto na utoaji wa dawa za minyoo kwa watoto.
Akiwasilisha taarifa ya uzinduzi wa Lishe Mratibu wa Lishe Emma Kalolo amesema lengo la mwezi wa Afya na Lishe ni kuboresha Afya na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa kwa watoto. Amesisitiza kuwa Wilaya nzima inatarajia kutoa chanjo hizo za matone na dawa za minyoo kwa watoto 114,441 hivyo amewaomba wazazi waliofika kituoni hapo kuwa mabalozi kwa wazazi wengine kuhakikisha wanapeleka watoto kwenye vituo vya Afya ili waweze kupata dawa hizo.
Akihitimisha uzinduzi huo Mkurugenzi amesema “Huduma za Mwezi wa Afya na Lishe ni muhimu kwa ukuaji na Maendeleo ya mtoto,tumfikie kila mtoto popote alipo ili watoto wetu wapate kinga za Afya bora”
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.