Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi.Happiness Msanga amefungua mafunzo endelevu kwa Walimu MEWAKA yanayotarajiwa kufanyika kuanzia leo Juni 19 hadi Juni 22,2023 katika Shule ya Msingi Kakora.
Akifungia mafunzo hayo Mkurugenzi amewataka Walimu kushiriki kikamilifu Ili kupata Elimu iliyokusudiwa kuwafikia Walimu wote.
" Mafunzo haya yamekuja kwa wakati mwafaka, mnaenda kujifunza mbinu za ufundishaji, matumizi ya teknolojia katika kuboresha Elimu, lakini pia mtajifunza matumizi sahihi ya kishikwambi"
Amewasiitiza Walimu hao kujifunza kwa umakini Ili kwenda kuwa mabalozi kwa Walimu ambao hawajapata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo, kwani Kila Shule wameshiriki Walimu wawili ambao watakwenda kuwafundisha Walimu wengine
Pia amesisitiza kutumia teknolojia kwa malengo sahihi ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji " tutumie teknolojia kwa kuongeza taaluma, vishikwambi vitumike kusaidia kuboresha Elimu"
Bi. Happiness amesisitiza nidhamu kwa walimu wote shuleni na mtamani" nidhamu ikipungua tu kila kitu kinaharibika kwahiyo mzingatie nidhamu"
Akiwasilisha taarifa ya mafunzo hayo mratibu wa MEWAKA Bi. Suzana Raphael amesema MEWAKA ni mafunzo endelevu ya Walimu kazini ni mkakati wa utekelezaji wa kihunzi cha mewaka kilichoandaliwa na wizara ya Elimu ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika Shule za msingi. Lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi,ufanisi na kutekeleza mtaala unaozingatia ujenzi wa umahiri kwa walimu.
Walimu wanaoshiriki mafunzo hayo wameishukuru Serikali kwa kuleta mafunzo hayo na wameahidi kwenda kuyafanyia kazi" tutafuatilia mafunzo haya vizuri na baada yamafunzo sisi ndio tunakwenda kuwafundisha wengine kwahiyo tutayazingatia " Bernad Njelekela Nolascus
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.