Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Bibi Pendo A. Malabeja amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kutumia Fedha za Ruzuku ya Maendeleo (CDG), Malipo kwa ufanisi (P4R na RBF)) katika maeneo mbalimbali ambayo miradi hiyo inatekelezwa.
Katika ziara yake, Mkurugenzi Mtendaji, aliweza kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika shule ya msingi Kiliwi, Shule ya Sekondari Bupamwa, Kituo cha Afya Mwamashimba, Shule ya Sekondari Mwamashimba, Shule ya Sekondari Talo, Zahanati ya Manawa, Kituo cha Afya Malya na Eneo la Maegesho ya Magari Hungumalwa.
Akiwa katika ziara hiyo,Bibi Pendo A. Malabeja alisisitiza na kuwaelekeza wasimamizi wa miradi kuwa Fedha za miradi ya maendeleo zilizopatikana zitumike katika miradi ambayo ni kipaumbele ili iweze kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Aliyasema hayo wakati wa kikao kifupi kilichofanyika katika shule ya Sekondari Mwamashimba
Aidha Bibi Pendo alimuagiza kaimu Mhandisi wa Ujenzi Ndugu Edwin Machumu kuhakiksha michoro ya mabweni ya shule ya sekondari mwamashimba inapatikana haraka iwezekanavyo ili mradi huo uweze kuanza na kumalizika kwa wakati.
Naye Afisa Elimu Sekondari Ndg Lawi Kajanja aliwaagiza Wakuu wa shule kuhakikisha wanatunza kumbukumbu za miradi kwa kufungua jalada la kila mradi.
Sanjari na maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkaguzi wa Ndani Ndg Maro Kenyuko aliwataka Watendaji Kata na Vijiji kuhakisha wanasoma taarifa za mapato na matumizi kwenye mikutano na vikao vya ngazi ya chini ili kuondokana na migogoro isiyo na msingi na kuhakikisha kila mmoja ana daftari la kumbukumbu/maelekezo.
Bibi Pendo A. Malabeja aliupongeza uongozi wa Zahanati ya Mwamashimba chini ya usimamizi wa Dkt. Paul Swakala kwa namna walivyosimamia vizuri ukamilishaji wa jengo la upasuaji ambalo litapunguza vifo vya mama na mtoto chini ya miaka mitano vinavyotokana na uzazi.
Mkurugenzi mtendaji, alihitimisha ziara yake kwa kuendelea kuwasisitiza Wakuu wa shule na waganga wakuu wa vituo vya afya kuhakikisha fedha za miradi zinatumika kama zilivyopangwa na miradi inakamilika kwa wakati bila kuwa na kisingizio chochote.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.