Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bibi Pendo A. Malabeja amefungua mafunzo ya mfumo wa Uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ujulikanao kwa Kiingereza kama Facility Financing Accounting and Reporting System (FFARS) kwa Mhasibu wa Hospital ya Wilaya, Wakuu wa Vituo vya Afya na Waratibu Elimu Kata yaliyotolewa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma yaani Public Sector System Strengthening (PS3) katika Ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) Kwimba tarehe 12/06/2017.
Akifungua mafunzo hayo; Bibi Pendo A. Malabeja amewaomba washiriki wa Mafunzo kuzingatia mafunzo hayo kwa umakini wa hali ya juu kwani watakwenda kufundisha watumishi wa Mamlaka za Serikari za Mitaa kwenye vituo vya kutolea huduma (Zahanati,Shule za Msingi na Sekondari)
Kwa upande wake mshauri wa masuala ya fedha (PS3) Bwana Martin Lawi amewataka washiriki wa mafunzo wawe kitovu cha mabadiliko kwa ajili ya mifumo na kuhakikisha taarifa za fedha zinaandaliwa kwa usahihi na zinatumwa kwa wakati makao makuu ya wilaya kila mwezi na kila robo ya mwaka.
Aidha mshiriki wa Mafunzo Bwana Jackson John Stephano ambaye ni Mratibu Elimu Kata ya Ngudu amesema mafunzo yamewajengea uwezo wa kutosha kwa upande wa “manual” hivyo basi wanahitaji mafunzo mengine kwa upande wa Kielektroniki kwa ajili ya ufanisi zaidi.
Washiriki wa Mafunzo ya mfumo wa Uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma wakisikiliza kwa makini Mada zinazofundishwa na wakufunzi.
Kwa kuhitimisha mafunzo hayo Mratibu wa PS3 Halmashauri ya wilaya ya kwimba Bwana Yohana Mhandikila ametoa shukrani zake kwa watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), pamoja na Mradi wa PS3, na wadau wote waliohakikisha mfumo huu unakuwepo, ambao ni: Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Halmashauri ya wilaya ya Kwimba ina jumla ya vituo vya afya vitano (05), Zahanati Aarobaini na nne (44) ,Hospitali moja (01), Shule za msingi mia moja hamsini na moja (151) na Sekondari thelathini na tano (35) Mafunzo haya yatasaidia kuhakikisha watoa huduma katika vituo wanapata ujuzi wa kutosha katika usimamizi wa fedha na kutoa huduma bora kwa wananchi wote na jamii zenye uhitaji.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
13/06/2017
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.