Mkurugenzi wa Shirika la AMREF Bi.Florence Temu amefanya ziara Kwimba, kukagua maendeleo ya Mradi wa ustawi wa Mwanamke , unaofadhiliwa na AIRISH AID, ambao umewezesha mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 123 kutoka vijiji na mitaa ya kwimba , wahudumu hao wamewezeshwa mafunzo ya mama na mtoto, uhamasishaji juu ya uchanjaji wa chanjo ya korona na mafunzo kiganjani kwa kutumia Mfumo wa Leap.Ziara hiyo imefanyika tarehe 16 mei,2022 katika Hospitali ya Ngudu ambapo Mkurugenzi wa Amref ameambatana na VIongozi wa Mkoa , viongozi wengine na wafanyakazi wa Amref.
Ziara hiyo ambayo ililenga kutoa Elimu juu ya utumiaji wa mfumo uitwao Leap,mfumo unaolenga kutoa mafunzo kwa wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii ili waweze kutoa huduma sahihi kwa wagonjwa hasa watoto na wanawake wajawazito.
" Leap ni mfumo ambao unamsaidia zaidi mwanafunzi kujifunza kupitia simu yake ya mkononi, Mwanafunzi anajifunza kupitia ujumbe na sauti na pia mfumo huu unampa nafasi ya kushirikiana na wenzake ambao wapo kikundi kimoja yaani (Group chati) mbali na hivyo mwanafunzi kila atakapo maliza mada atatakiwa kufanya mtihani na endapo atapata chini ya alama 80 basi atarudia somo aliloshindwa" alisema Gaitano
Mfumo wa Leap unarahisisha sana katika kuwafanya wahudumu wa afya wawe na mafunzo endelevu na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa jamii kwa sababu muhudumu anaweza kupata mafunzo bila kujali eneo alipo lakini pia anaweza akapata mafunzo muda wowote bila gharama. Anaitaji kuwa na simu tu na haitaji kuwa na bando la mtandao wala kuchangia gharama yoyote alieleza Elia Msegu Meneja wa mradi wa Ustawi wa Mwanamke
Nae Mkurugenzi wa AMREF Bi.Florence Temu akapata nafasi ya kueleza juu ya umuhimu wa utoaji Elimu kwa wahudumu hao
" niombe tushirikiane katika kuhakikisha tunatoa Elimu kwa jamii husika na pia tuhakikishe tunapokwenda kutoa huduma tuwe na vifaa vyote, Bi Florence amewasisitiza Wahudumu hao kutoa huduma kama walivyojifunza ili huduma hizo ziwe na tija kwa jamii.
Mbali na hivyo Mkurugenzi aliapata muda wa kujionea namna wanafunzi( wahudumu wa Afya ngazi ya jamii) wanavyoweza kutumia mfumo huo wa leap, kisha ametoa pongezi kwa watoa huduma hiyo " niwapongeze Kwimba kwanilivyoona kupitia kwa mwanafunzi huyu ni hakika mnatoa Elimu inayofaa kwa mahitaji ya wahudumu hawa"
Shirika la AMREF linatoa elimu kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya hasa huduma za Mama mjamzito na watoto ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vitokanavyo na uzazi na kuboresha ustawi wa mwanamke.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.