Mkutano Mkuu wa kufunga hesabu za Halmashauri umefanyika leo Agosti 25,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba huku Halmashauri ikionekana kupaa katika ongezeko la mali za kudumu kutoka mali zenye thamani ya bilioni 65.8 kwa mwaka 2021/22 hadi bilioni 71.9 kwa mwaka 2022/23.
Ongezeko hilo limetokana na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya, Zahanati, madarasa, vyoo na miundombinu mingine.
Akiwasilisha taarifa ya hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2023 Bi. Happiness Msanga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba amesema Halmashauri inaedelea kusimamia mifumo ya fedha Ili kuhakikisha fedha zote zinatumika na kufanya kazi katika malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Mkurugenzi amesisitiza kuwa Halmashauri imeongeza mali za kudumu, pia imepunguza kiwango cha madeni ya muda mfupi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Lameck Hole akifungua mkutano huo amewapongeza wataalamu kwa kazi nzuri ya ufungaji wa hesabu na ameipongeza Halmashauri kwa kupunguza madeni pia ameshauri madeni yaendelee kulipwa Ili mwaka wa fedha ujao kuwe na taarifa tofauti.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.