MKUU WA MKOA AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE MPYA MWALULYEHO NA KITUO CHA AFYA HUNGUMALWA
Wananchi wa Kijiji cha Chasalawi katika Kata ya Bupamba wilayani Kwimba wamechangishana na kununua eneo la Ardhi lenye ukubwa wa Hekari Nane kwa ajili ya kujenga Shule ya Msingi ili kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya Kilomita tano.
Hayo yamebainishwa leo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Adam Malima ambapo Kiongozi huyo amekagua na kuweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Miundombinu ya vyumba vya Madarasa 9, Matundu ya Vyoo 30 na Jengo la Utawala kwenye shule ya Msingi Mwalulyeho yanayotekelezwa kwa Tshs. Milioni 250 zilizotolewa na serikali kuu.
Amesema, wananchi wa kijiji hicho wameonesha kuwa na kiu ya maendeleo na uzalendo kwa kuamua kwa hiyari kununua eneo na kuanzisha Ujenzi kabla ya serikali kuwaletea mawazo na akatumia wasaa huo kuwaahidi kuwatimizia ndoto yao ya kupata shule kwa kuhakikishia kukamilika kwa ujenzi mapema mwezi Aprili 2023.
"Nawashukuru sana kwa kujitolea kuanzisha mradi wa maendeleo na ukiona jamii inafanya haya kwa hiyari basi ujue eneo hilo wananchi wake wanajitambua sana maana hakuna mtu anayeweza kujenga shule ili asome mwanae pekee bali ni kwa ajili ya jamii nzima., hongereni sana." Malima.
Aidha, ametoa rai kwa wazazi wa kata ya Bupamwa kuhakikisha wanawapeleka watoto shule hususani wa kike ili kuwatimizia ndoto ya kujitegemea na akawasihi kuacha tabia ya kuwaozesha kwa kishawishi cha kupata mifugo kama mahari huku alisema wakifanya hivyo wataharinu jamii nzima ya sasa na baadae.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ngw'ilabuzu Ludigija ametumia wasaa hup kumshukuru Mhe Rais kwa kuwaletea fedha za Ujenzi wa shule hiyo na akawapa konvole wananchi kwa kuamua kujiletea maendeleo wenyewe bila kusubiri na akawataka kuendelea na tabia hiyo njema.
"Rais Samia hakukosea kukuleta Mhe. Malima Mkoni mwanza maana tutanufaika sana na Uongozi wako maana una uchungu wa maendeleo ndio maana pamoja na kufanya ziara za kusikiliza kero za wananchi unahakikisha unakagua kila mradi hadi iliyopo maeneo ya mbali kiasi hiki." Me. Sabana Salinje, Mwenyekiti wa CCM Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.