" Wataalam tuwaze kwa niaba ya vikundi, tuwasaidie kujua kitu gani wafanye ili fedha wanayokopa iweze kuwainua kiuchumi"
Haya yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel wakati wa mafunzo ya kujenga uwezo wa uratibu na usimamizi wa mfuko wa maendeleo ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu unaotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani yaliyofanyika leo tarehe 16 May, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Mhandisi Gabriel amesisitiza kuwa elimu itolewe kwa vikundi vinavyohitaji kukopa ili wanapopata mikopo wajue namna nzuri ya kwenda kuizarisha hiyo fedha ili iwasaidie kujikwamua kimaisha. Pia amewataka Wataalamu kutoa ushauri kwa vikundi na kuwasimamia katika kazi wanazozifanya ili kuhakikisha fedha hizo zinafanya kazi iliyokusudiwa. Aidha Mkuu huyo amesisitiza ushirikiano kwa viongozi wote ndani ya Wilaya hiyo na amewataka viongozi hao kutimiza wajibu wao ili kupata matokeo chanya ya kazi zao.
"bila jasho huwezi kupata matokeo chanya, niwaombe mkafanye kazi kila kiongozi kwa nafasi yake tutafanikiwa" amesema Mhandis Gabriel
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi baada ya mafunzo hayo amewaelekeza viongozi wote kwenda kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa
"tuache kufanya kazi kwa mazoea kila siku nasisitiza tufanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa"
Wajumbe wa mafunzo hayo wakiwemo Waheshimiwa Madiwani Wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwani kupitia mafunzo hayo wameweza kujua sheria zinazotakiwa kuzingatiwa kabla na baada ya kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, vilevile wamefaham kuwa wanao wajibu wa kutoa Elimu kwa Wananchi kuhu mikopo inayotolewa na Halmashauri inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.