Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe:John Mongela akagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba eneo la Icheja kata ya Ngudu wakati akielekea kwenye kikao maalum cha baraza la madiwani cha kujadili na kukagua hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.Mhe:Mongela amewashauri viongozi wanaosimamia ujenzi huo kuongeza mafundi na wafanyakazi wengine ili ujenzi huo uweze kukamilika kwa wakati.Aidha amemtaka Mkuu wa Wilaya Mhe:Senyi Ngaga na Mkurugenzi Bib,Pendo Malabeja kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinapatikana kwa wakati,majengo yote yanayotakiwa kujengwa OPD,maabala,utawala na jengo la mionz yajengwe kwa pamoja ili ujenzi ukamilike kwa pamoja.
Katika kikao maalum cha baraza la madiwani cha kupitia na kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Mhe: Mongela ameipongeza Halmashauri ya Kwimba kwa kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo na akataka hali hii iendelee ili Halmashauri isiwe na hoja za kiukaguzi miaka ijayo.Aidha Mhe: Mongela ameitaka Halmashauri kuzingatia risiti za EFD wakati wa malipo yote na amesisitiza usimamizi mzuri wa POS(mashine za ukusanyaji wa mapato) ili kuongeza mapato ya Halmashauri.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.