Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Kigoma Malima afungua maonyesho ya nanenane kwa kuwataka wakulima kutumia kanuni bora za uzalishaji ili kufikia mwaka 2030 Tanzania tuwe tumefikia asilimia 10 za uzalishaji kwenye pato la Taifa.
Ufunguzi huo umefanyika leo tarehe 4,Agosti 2022 katika viwanja vya Nyamhongolo Mwanza. Akifanya ufunguzi huo Mkuu wa Mkoa amewasisitiza Wananchi kutumia fulsa za uwepo wa ziwa na mashamba kwaajili ya kuendeleza kilimo na ufugaji wa kisasa
“ Mkoa wa Mwanza unaeneo kubwa linalowezesha shughuli za uvuvi hasa kwa kutumia vizimba, niwashauri mtumie ziwa kufuga kisasa ili kupitia ufugaji huo uchumi wetu uongezeke zaidi” Aidha amesisitiza Elimu kuhusu ufagaji wa kisasa itolewe kwa vikundi vya vijana ili iwasaidie kujiendeleza kiuchumi.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameshauri taasisi za fedha zitumike ili kupata mikopo ya kuendeleza shughuli za kilimo ili zisaidie kuimalisha usalama wa chakula na kuongeza kipato kwa wakulima na wafugaji.
Mkuu huyo amesema Lengo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha viwanda vinavyotumia bidhaa za kilimo vinaongezeka zaidi ili mazao yanayozalishwa yaongezewe dhamani na ajira kwa vijana ziongezeke.
Maonyesho ya nanenane yamelenga kuwaonyesha wakulima na wadau wengine kuwa kilimo kinaweza kumfikisha mkulima mahali anapotaka kufika kama ataamua kulima na kufuga kisasa.
Mheshimiwa Malima ameitumia nafasi hiyo kutoa elimu ya sensa kwa wananchi huku akisisitiza umuhimu wa takwimu za idadi ya watu na makazi ili kuirahisishia Serikali kupanga mikakati ya maendeleo
” niwaombeni wote mjipange kushirki siku ya Sensa, wote tutoe ushirikiano kwa wakusanya takwimu”
Akikagua mabanda ya maonyesho amepita banda la Kwimba ambapo amesisitiza elimu ya kilimo cha Maboga makubwa, Pamba, dengu na mazao mengine itolewe kwa Wananchi ili kilimo hicho kilete tija kwa Wananchi.
“ nitamfatilia huyu mama anayelenga kupanda hizi mbegu za Boga ili nione kama atapata maboga makubwa kama haya mnayotuonyesha watu wa Kwimba, toeni elimu na wasaidieni wakulima wanaolenga kufanya kilimo cha mazao yanayopatikana Kwimba” amesema Adam Malima
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.