Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla Leo Novemba 27,2023 amefanya ziara Wilayani Kwimba kwenye viwanja vya Stendi ya zamani Ngudu kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Akifungua mkutano wake Mhe. Makalla amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inawajali sana wananchi wa Kwimba kwani imeleta Miradi lukuki ya Maendeleo ukiwemo Ujenzi wa Barabara ya Lami ya Kwimba -Magu (Km 10).
Ameongeza kuwa pamoja na ujenzi wa Barabara hiyo ambayo mkandarasi ameshapatikana, Iko miradi mingi inayoendelea kutekelezwa ikiwa ni pamoja na mradi wa maji Sumve, mradi wa maji Hungumalwa wenye bilioni kumi na miradi mingine.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa ameonesha kutokua na imani na Mkandarasi anayejenga jengo la kisasa la Makao Makuu ya Halmashauri kutokana na kusuasua katika ujenzi wake pamoja na uwepo wa fedha za ujenzi ambazo ameshapatiwa na kumtaka kujitafakari kabla hajachukua maamuzi mengine.
Aidha, amewataka watendaji wa idara ya ardhi na wengine halmashauri hadi kwenye ngazi za vijiji kuwa na ratiba yenye tija ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa wakati na kuhakikisha migogoro hususani ya ardhi inakomeshwa.
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija alifafanua kuwa ameshawasikiliza zaidi ya wananchi 400 na kwamba amebaini kuwa sekta ya ardhi imekua na migogoro zaidi hususani inayosababishwa na Mashamba ya urithi hivyo amewataka wananchi kufuata taratibu kwenye kuridhi mali ili kuepusha adha hizo.
Mheshimiwa Makalla ametatua kero mbalimbali zikiwemo kero za ardhi, wastaafu, maji, umeme,barabara na kero nyingine.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.