Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo novemba 28, 2023 amezindua Miundombinu ya Kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari Mwamashimba wilayani Kwimba iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 600.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, Mhe. Makalla ameupongeza uongozi wa shule hiyo na halmashauri kwa usimizi mzuri wa Mabweni 3, Vyumba vya Madarasa 8 na Matundu ya vyoo 13 utakaosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa na mabweni.
"Nimeona mabweni mazuri yenye mpangilio mzuri wa vitanda, madarasa na matundu ya vyoo vyote kwenye hali ya usafi na unadhifu mzuri, tumieni jitihada hizi za uboreshaji kutulia na kusoma kwa bidii na nina imani baadae tutawapata viongozi wazuri kutoka kwenye shule hii." Makalla.
Vilevile, Mhe. Makalla ameagiza kulindwa kwa eneo la shule hiyo kwa kutambua na kuweka mipaka na kuweka uzio ili kuwalinda wanafunzi na kuepusha migogoro ya ardhi inayosababishwa na wananchi kuingia kwenye maeneo ya taasisi hususani yasiyo na mipaka inayofahamika.
Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amemhakikishia kiongozi huyo wa Mkoa kuwa ufaulu utaongezeka kwani pamoja na kuondoa msongamano wanafunzi kwenye shule hiyo watapata fursa nzuri ya kusoma kwenye mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa wanafunzi wa kidato cha tano na sita wapo zaidi ya Mia 600 lakini kwa uwepo wa mabweni haya hivi sasa kila mwanafunzi atalala kwenye kitanda chake, hakuna tena msongamano bweni wala darasani." Amefafanua Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Happness Msanga.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa amezindua Shule mpya ya Msingi Mwalulyeho katika kijiji cha Chasalawi Kata ya Bupamwa iliyojengwa kwa zaidi ya Milioni 250 ambayo imesaidia kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kuelekea shule ya Chasalawi.
"Kama mlikua na kiu ya kupata shule, sasa mmejengewa tumeiona ni nzuri yenye samani za kutosha, basi waleteni watoto kwenye hii shule wasome maana hawa 303 wamehamia hivyo wazazi hakikisheni watoto wote wanakuja shule ifikapo mwezi januari 2024 asibaki nyumbani hata mmoja mweye umri wa kuanza shule" amesema Makalla
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.