Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe: Senyi S.Ngaga amefanya ziara ya kikazi kuwasikiliza wananchi mahitaji na changamoto zinazowakabili katika Tarafa ya Nyamilama,amebain uhaba wa madawati katika shule ya Msingi hivyo kuwataka wenyeviti kutengeneza madawati hayo na ifikapo mwezi wa tano yakabidhiwe.Aidha amewataka viongozi wa vijiji waachane na migogoro isiyo ya msingi na wajikite katika kazi za kuleta maendeleo katika vijiji vyao,pia amewataka viongozi wa kila Kijiji kuaandaa heka mbili kwaajili ya shamba darasa la kuotesha miche 200 ya korosho.
Katika ziara hiyo Mhe: Ngaga amebaini changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule za msingi na sekondari na huduma za Afya kulegalega kwa baadhi ya zahanati na vituo vya Afya hivyo akamtaka Mganga mkuu wa wilaya kushugulikia changamoto hizo za kiafya.Aidha Mkuu amewashauri wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya (CHF) iliyoboreshwa ili kurahisisha gharama za matibabu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.