Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amefungua mafunzo ya Mgambo kwa vijana 69 ambapo wakike walikua tisa na wakiume 60,mafunzo hayo yamefunguliwa jana tarehe 5 Julai, 2022 katika kijiji cha Nyambiti Kata ya Nyambiti.
Akifungua mafunzo hayo Mheshimiwa Samizi amewataka vijana hao kuwa na nidhamu, kujituma na ushirikiano katika kila wanachokifanya na wanachoelekezwa na wakufunzi wao. Pia amewataka baada yamafunzo hayo wakaanzishe vikundi vya ujasiliamari vitakavyowawezesha kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri ili waweze kufanya bishara zitakazowainua kiuchumi.
"msingi wa mafanikio na maendeleo ni nidhamu, nidhamu ni ufungio wa mambo mengi, fanyeni mazoezi, wasikilizeni wakufunzi wenu mtafika mbali" amesema Samizi
Aidha Mkuu wa Wilaya ameitumia nafasi hiyo kuwataka Wananchi kuweka akiba ya chakula kwani wananchi wengi wameonekana kuuza vyakula hadi vile vya akiba kitu kitakachopelekea njaa. Amesisitiza kuwa Wananchi wafahamu kuwa hakutakuwa na chakula cha msaada kwahiyo kila familia wahakikishe wanatunza akiba ya chakula.
"Wananchi mnachokifanya siyo sahihi mnauza chakula chote, mnafulahia bei lakini mnachokitengeneza ni wimbi la njaa, sasa nawaelekeza kila familia kutunza chakula, mnapouza mazao yenu hakikisheni mnatunza yale yatakayotosheleza hadi msimu mwingine"
amesema Samizi
Naye Mshauri wa Mgambo Meja Gadiel Mndeme akisoma taarifa ya mafunzo hayo amesema vijana hao watapewa mafunzo mbalimbali yakiwemo mafunzo ya kwata, masomo ya uraia, mbinu za kivita, usomaji wa ramani, somo la uhamiaji, ujanja wa polini, mafunzo ya silaha ndogondogo, somo la usalama, uokozi na rushwa. Amewashauri vijana ambao bado hawajajiunga na mafunzo hayo kwenda kujiunga kwani ni mafunzo yatakayowasaidia vijana kuwa wajuzi wa mambo mbalimbali na wakakamavu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.