Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi ametembelea mashamba ya Pamba kuona kama Wakulima walifanyia kazi Elimu waliyopewa ya kilimo bora cha Pamba, iliyotolewa na Balozi wa Pamba akishirikiana na Mkuu wa Wilaya na Wataalamu wa Kilimo. Ukaguzi huo umefanyika tarehe 15-16 Feb, 2022 ambapo Wakulima wengi wamefurahia kutembelewa katika mashamba yao.
Aidha Wakulima wengi wameonekana kuzingatia Elimu waliyoipata kwani wamelima kwa kuzingatia vipimo walivyoelekezwa,matumizi ya mbolea na kupalilia kwa wakati.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ametoa mbolea kwa wakulima wote waliotembelewa na pampu kwa baadhi ya wakulima.
Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wakulima kunyunyizia dawa kwa wakati ili kuzuia wadudu wabaya wanaoshambulia vitumba vya Pamba. Wakulima wenye pamba nzuri wamepongezwa na kusisitizwa kuendendelea kulitunza zao hilo.
Aidha Mheshimiwa Samizi amewatia moyo wakulima ambao mashamba yao yamejaa maji kitu kinachopelea pamba kudumaa na kuharibika, amewataka kutokata tamaa na zao hilo.
Kilichomfurahisha zaidi Mkuu wa Wilaya nikuona Walimu wa Shule ya Msingi Ilula wakiongozwa na Mwalimu Juma Mpina wakijishughulisha na kilimo cha Pamba ambapo mashamba yao yameonekana kuwa na mazao ambayo yanatunzwa vizuri na hayajashambuliwa na wadudu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.