Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Johari Mussa Samizi amekemea tabia ya baadhi ya vijana wa Kijiji cha Shilembo kufanya matukio ya kihalifu ikiwemo kufunga barabara, kugombana, kuharibu miundombinu ya anwani za makazi na miundombinu mingine kwa kisingizio cha ulevi ( kulewa).
Ameyasema hayo leo tarehe 2,Novemba 2022 katika mkutano na Wananchi wa kijiji cha Shilembo uliofanyika katika Shule ya Msingi Mwamakelemo.
“ asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, ulimwengu ni Wananchi wote, hao vijana tutawafunza kwa kuwachukulia hatua hatuwezi kufumbia macho uhalibifu wa miundombinu ambayo Serikali imetoa fedha nyingi kuitengeneza” amesema Samizi
Katika mkutano huo viongozi wa Kijiji wametakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za uongozi vilevile viongozi wametakiwa kusoma mapato na matumizi ya kijiji kila wanapofanya mikutano.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka viongozi wa ulinzi shirikishi (Sungusungu ) kuendelea kufanya kazi na kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao kwa kuzingatia taratibu walizojiwekekea.
Vilevile Wananchi wameshauriwa kuhakikisha wanapata lishe bora hasa kwa watoto chini ya miaka mitano ili kuhakikisha usalama wa Afya zao na kuwakinga na utapiamlo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.