Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Ng'wilabuzu Ludigija amewapongeza Wananchi wa Kata ya Sumve kwa kujitokeza kwa wingi kuchimba msingi wa jengo la wazazi, ameyasema hayo leo April 13,2023 wakati akishiriki zoezi la kuchimba msingi kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa kituo cha Afya Budushi Sumve
"niwapongeze kwa kujitokeza kwa wingi kwenye uchimbaji wa msingi,kazi hii mliyoifanya nikubwa sana na nimfano wa kuigwa lakini nimpongeze Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kutenga fedha za mapato ya ndani millioni 300 kwaajili ya kuanzisha ujenzi wa hiki kituo cha Afya, Sasa leo tunachimba msingi wa jengo la wazazi litakalotekelezwa kwa million 136 fedha za Mpango wa kunusuru kaya masikini( Tasaf)"
Mkuu huyo amewataka Wananchi wote kuhakikisha wanawake wajawazito hawajifungui nyumbani kwasababu vituo vya Afya ni vingi vilevile ameutumia muda huo kuwashauri Wananchi kusomesha watoto wao hasa watoto wa kike Ili kuwawezesha kujitambua na kujiandalia maisha yao ya badae
" Rais wetu ametujengea madarasa mazuri mengi ya kutosha hakuna mzazi anayedaiwa dawati wala fedha ya darasa nyie ni kupeleka watoto shule Sasa pelekeni watoto wenu shule tena watoto wa kike wasomeshwe msifurahie kupokea mahali harafu mkawaharibia ndoto zao, niwambie kabisa atakayegundulika amekatiza masomo ya mtoto wa kike au amempamimba mwanafunzi tutamfunga" Ludigija
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewapongeza wananchi kwa kuendelea kutoa nguvu zao kushiriki ujenzi wa kituo hicho, vilevile ameshauri maandalizi ya vifaa vichache yafanyike Ili ujenzi wa majengo mengine unapoendelea, huduma za wagonjwa wa nje ziendelee kutolewa kwenye jengo la OPD ambalo limefikia hatua za mwisho za ukamilishaji.
Katika shughuli hiyo ameshiriki Mwenezi wa CCM Mhe. Shija Malando ambaye amewapongeza viongozi wote kwa kuendelea kufanyakazi na kutimiza maelekezo yaliyowekwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi
.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.