Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi leo tarehe 08/02/2022 amewaongoza Wananchi wa Kata ya Maligisu kuchimca msingi wa majengo manne na nyumba ya Mganga moja kwaajili ya ukamilishaji wa Kituo cha Afya kinachojengwa katika Kijiji cha Kadashi.
Jumla ya Milion 300 zimepokelewa kwaajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo hicho cha Afya ambapo majengo yanayotarajiwa kujengwa ni nyumba ya Daktari, theater, mochwari, kichomea taka na choo.
Kituo hicho kinayo majengo matatu yaani jengo la wagonjwa wa nje( OPD), maabara na jengo la Mama na Mtoto ambayo yako katika hatua za ukamilishaji. Utekelezaji wa majengo haya matatu umetumia nguvu za Wananchi na milion 205 fedha ya Serikali.
Akiongea na Wananchi baada ya kuchimba msingi Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wote kujitolea, kushiriki katika ujenzi, kulinda na kusimamia kazi zote zinazoendelea katika eneo hilo
" Kituo ni chetu sote hivyo tushirikiane kuhakikisha kituo hiki kinakamilika ili kianze kutoa huduma kwa Wananchi" amesema Johari
Mkuu huyo amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha nyingi za miradi mbalimbali inayotekelezwa Wilayani hapa ikiwemo huu wa Kituo cha Afya Maligisu.amesisitiza kuwa ujenzi wa kituo hiki ni muhimu kwa Wananchi wa Maligisu kwani wanatembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya hivyo linapaswa kuwa jukumu la kila mkazi na kiongozi wa Wilaya hii kuhakikisha kituo kinakamilika na kuanza kutoa huduma.
Wananchi walioshiriki uchimbaji wa msingi wamemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha hizo kwaajili ya ukamilishaji wa kituo hicho, wanamuomba Mheshimiwa Rais aemdelee kuleta fedha za miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya rami ya Hungumalwa- Ngudu - Magu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.