Akifunga mafunzo ya Mgambo leo tarehe 14/11/2020 Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Saimon Ngaga amewaasa wahitimu wa Mgambo kutumia ujuzi walioupata katika kufanya kazi za kuwaletea maendeleo siyo kutumia ujuzi huo kutenda uhalifu.Aidha Mkuu wa Wilaya amesema amefurahishwa na wahitimu hao ambao wanawake ni watano na wanaume 68 kwani wamehitimu wote hakuna hata mmoja aliyekimbia mafunzo hivyo amewasisitiza kuwa ukakamavu na utimamu wa mwili walioupata wakautumie vyema,pia amewataka kuwa tayari kujitolea pale shughuli zinapojitokeza kwenye jamii zinazohitaji nafasi zao kama Mgambo.
Wakisoma risala yao wahitimu hao mbele ya Mgeni rasmi wameiomba Serikali kuwakumbuka pindi nafasi za kwenda JKT ( Jeshi la Kujenga Taifa) zinapojitokeza, wameomba wapewe kipaumbele ili waweze kwenda kuendeleza ujuzi walioupata.
Wahitimu hao wakiongea na waandishi wa habari wamesema wanawashauri watu wengine kujitokeza kujiunga na mafunzo ya Mgambo kwani ni mafunzo mazuri na hakuna mtu aliyedhurika kama wengine wanavyodhani,pia wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kupata ajira hasa za ulinzi na kufanya kazi nyingine zinazohitaji ukakamavu na ujuzi walioupata.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.