Ameyasema hayo leo tarehe 11/02/ 2022 kwenye Kongamano la Walimu wa kike,lililofanyika kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu Kwimba.
Katika kongamano hilo Mkuu wa Wilaya Mhe. Johari Samizi aliyekuwa Mgeni rasmi katika tukio hilo amewaeleza majukumu makuu matano ya mwalimu ambayo ni jukumu la malezi kwa mtoto(mwanafunzi) amesema bila malezi bora ya Wanafunzi kinaweza kutokea kizazi goigoi, kisichoweza kufanya mambo vizuri hivyo amewataka kutimiza jukumu hilo kwa ufasaha.
Aidha Mheshimiwa Samizi amewasisitiza kuitendea haki Taaluma yao kama inavyotakiwa kwa kufundisha kwa moyo wote bila kujali mazingira na changamoto zinazojitokeza katika mazingira yao ya kazi. Amesema kuitendea haki taaluma hiyo kitu kitakachowafanya kutambulika na kuheshimiwa na jamii kwa kazi hiyo,
" Walimu wa zamani walikua wanajipambanua kiasi kwamba walijulikana sana kwa kuwa waliipenda kazi yao na waliitenda kwa moyo niwaombe na nyie mfundishe watoto wetu kwa moyo na mjipambanue kwa kazi yenu jamii iwatambue na itambue mnachokifanya" amesema Samizi
Majukumu mengine ni kuwajibika kwa jamii, kuwajibika kwa mwajiri na kuwajibika kwa Taifa. Mkuu huyo amesisitiza kuwa Walimu ni kiyoo cha jamii kwani Taifa la kesho litatokana na malezi bora ya Walimu kwasababu wanafunzi wanatumia mda mwingi wakiwa na Walimu kuliko wazazi wao hivyo Ualimu wao utumike vyema kuifanya kazi ya kulijenga Taifa na kutengeneza viongozi bora wa badae.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.