Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Johari Samizi jana tarehe 7/3/2022 amekagua miradi ya maji mitatu na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Ng'uliku.
Katika hafla hiyo Mhuu wa Wilaya amewataka wataalamu kutoka RUWASA kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu miradi inayoendelea hasa ile inayotekelezwa na wakandarasi ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Akisoma taarifa ya miradi hiyo meneja wa RUWASA Wilaya ya Kwimba amesema mradi wa Ibindo unatekelezwa kwa fedha za UVIKO-19 ambapo milioni 505 zimeshapokelewa na mkandarasi yupo kazini kwaajili ya kujenga tanki kibwa litakaloweza kuhifadhi maji ya kutosha maeneo hayo.Amesema tangi la Izizimba B nalo linajengwa na mkandarasi kwa fedha za UVIKO -19 ambapo milion 315.1 zitatumika kujenga tangi la lita 135,000 na na kutandaza mabomba kwa Wananchi.
Meneja huyo amesisitiza kuwa ujenzi wa tanki la ng'uliku umekamilika na hivyo mtandao wa maji umeongezeka katika kijiji hicho na vijiji jirani.
Wananchi wa maeneo hayo yanayotekeleza miradi ya maji wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuwafikishia majo katika vijiji hivyo
" Tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa kutuletea maji kijijini kwetu tena maji ya ziwa victoria kweli Mama ameamua kututua ndoo kichwani wanawake wenzake tunamshukuru sana" amesema Milembe Charles mwananchi wa kijiji cha Ng"uliku
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.