Wanawake wajawazito waaswa kuacha tabia za kujifungua nyumbani badala yake wafike kwenye vituo vya Afya vilivyo karibu yao Ili wajifungue katika mazingira salama.
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ngw'ilabuzu Ludigija Leo Machi 4,2023 wakati akizingua huduma za Afya katika Kituo cha Afya Kadashi
" niwashauri Wananchi wote hivi vituo vya Afya mvitumie, hatutarajii kusikia wanawake wanajifungua nyumbani acheni tabia hiyo ya kuhatarisha maisha yenu na watoto, njooni mjifungue kwenye vituo vya Afya, Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewajali Wananchi ametujengea kituo cha Afya kitumieni vizuri" amesema Ludigija
Katika Hafla hiyo ameshiriki Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe.Kasalali Mageni ambaye amewashukuru Wananchi Kwa kuanzisha ujenzi wa Zahanati ambayo baada ya kuanzisha Waziri Mkuu alishauri ipandishwe hadhi na kuwa kituo cha Afya." niwapongeze Wananchi wa Kadashi tumepambana sana hadi kituo kimekamilika, Sasa kituo hiki mkitunze ili kiweze kutoa huduma zilizokusudiwa" Kasalali
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi.Happiness Msanga akiwasilisha taarifa ya mradi huo ameishukuri Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwaajili ya kukamilisha kituo hicho
" Imekuwa historia Kwa sababu ujenzi ulianza tangu mwaka 2012 Kwa nguvu za Wananchi na baadae Serikali ilileta fedha Kwa Awamu tofauti ambazo zimewezesha kukamilika Kwa kituo hiki" Msanga
Hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali ambao wote wamepongeza jitihada za Mheshimia Rais za kuwaletea maendeleo Wananchi" nampongeza na kumshukuru Mheshimia Rais kwa kuendelea kuleta fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo,pia niwaombe wanawake muache kujifungua nyumbani" Thereza Lusangija Mwenyekiti wa Halmashauri
Wanchi wa Kata ya Maligisu wameishukuru Serikali Kwa kuwasogezea huduma za Afya " tunaishukuru sana Serikali Kwa kutuletea huduma zaAfta tulikuwa tunateseka hasa wanawake kujifungulia njiani na wakati mwingine wazazi wamefariki, Sasa hiki kituo kitatusaidia s sana" amesema Milika Chananja
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.