Mheshimiwa Johari Mussa Samizi amefanya uzinduzi wa anwani za makazi kwa kubandika namba kwenye Nyumba na kuweka bango la kuonyesha jina la Mtaa au barabara. Zoezi hili limefanyika leo tarehe 16 Feb, 2022 katika barabara ya Klasta na Fimbo.
Aidha Mheshimiwa Samizi amewaomba Wananchi wa Wilaya ya Kwimba kujitokeza kupendekeza majina ya Mtaa wanayoyapenda na kujitolea kutengeneza vibao vya majina hayo ili kila mtu ashiriki katika kazi hiyo.
Mkuu huyo amesisitiza kuwa uwekaji wa anwani hizi za makazi ni muhimu kwani zitasaidia kurahisisha kufahamika kwa maeneo vilevile zitapunguza usumbufu uliokuwa unajitokeza pale mtu anapokuwa akielekea sehemu asiyoifahamu, kwani anwani hizi zikiishaingizwa kwenye mtandao zitamrahisishia mtu kutafuta mahali anapotaka kwenda kwa kutumia mtandao. Pia amesisitiza kuwa kukamilika kwa anwani hizi kutasaidia kurahisisha shughuli za Sensa.
" tengenezeni vibao vya majina yenu lakini yawe majina mazuri kwamaana ya majina yenye maana nzuri na yanayotambulika na kueleweka" amesema Samizi
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewapongeza wananchi kwa kujitokeza katika uzinduzi huo na amewashauri kutengeneza vibao vya majina ya Mitaa vyenye majina yao kwani kutengeneza vibao hivyo kutawafanya majina yao yaishi miaka yote hata kama wamiliki wa majina hawatakuwepo lakini majina hayo yataendelea kutumika.
" tengenezeni vibao vyenye majina yenu ili muweke alama ambazo hazitafutika ili ziwe kumbukumbu hata kwa vizazi vinavyokuja" amesema Msanga
Akitoa ufafanuzi wa zoezi hilo Afisa Ardhi wa Wilaya Ndugu Wickriph Benda amesema zoezi hili linawapa uhuru Wananchi kushiriki kwa kuchagua majina ya Mtaa na anayeweza kutengeneza kibao na kuweka majina ya Mtaa ameruhusiwa lakini majina yanayoruhusiwa niyale yenye maana nzuri, yasiwe ya kejeri na matusi bali yawe majina ya watu au kitu kinachopatikana katika eneo husika ili iwe rahisi kutambulika.
Uzinduzi huo umehudhuliwa na Wananchi, ambao wameona kukamilika kwa operersheni hiyo kutasaidia kujulikana kwa mitaa na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na nyingine nyingi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.