Mkuu wa wilaya ya kwimba Mhe.Johari Samizi amefanya ziara leo Juni 7,2022 katika Wilaya ya Misungwi kwa lengo la kujifunza namna ya kumalisha miradi.Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya kwimba ameambatana na kamati ya usalama Wilaya ya Kwimba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Ndugu Denis Kabogo na wajumbe wengine kutoka Halmashauri. Naye Mhe Veronica Kesi Mkuu wa Wilaya ya Misungwi akaungana nao ili kutembelea miradi ya Misungwi.
katika ziara hiyo wametembelea kituo cha Afya Cha Idetemya kilichopo Usagara,Daraja la Busisi pamoja na shule ya sekondari ya Sanjo wakilenga kupata mafunzo ya namna bora ya ukamilishaji wa miradi kwa wakati.
Baada ya ziara hiyo kukamilika Mkuu wa wilaya ya Kwimba ametoa pongezi kwa Mkuu wa wilaya ya misungwi kwa kuweza kukamilisha miradi" nitoe pongezi kwa Wilaya ya Misungwi kwa hatua mliyofika kwani miradi kwa asilimia kubwa imekamilika tofauti na kwimba,Kwimba bado tupo nyuma kidogo ukilinganisha na nyie Misungwi na ndio maana leo tumekuja kufanya ziara tujifunze namna ya kukamalisha miradi kwa haraka na kwa ubora zaidi natumaini Mimi na wajumbe wangu tumejione na tumejifunza kupitia miradi ya hapa misungwi"
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe Veronica Kesi akatoa neno" Mimi niombe sisi tupeane ushirikiano katika kujenga Mkoa wetu kwa kushirikiana katika miradi lakini pia tujenge mazoea ya kutembeleana ili tuweze kujifunza zaidi kwa vitendo na kufanya hivyo tutaijenga Mwanza yetu"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.