Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Mtemi Msafiri Simeoni amefungua Warsha ya kupitia na kupitisha mpango kazi wa wilaya ya kwimba katika Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na ushirika pamoja na idara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Tarehe 05/07/2017.
Tupambane kufa na kupona kuhakikisha vipaumbele vya Halmashauri vinatutoa hapa tulipo na tunasonga mbele, tuone wananchi wetu wanatoka kupitia vipaumbele vyetu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bibi Pendo A.Malabeja wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua Warsha hiyo.
Akifungua mafunzo hayo Mhe. Msafiri amesema Idara ya kilimo na mifugo ni muhimu sana katika wilaya ya kwimba hivyo amewaomba wataalam watumie warsha hiyo kujifunza na kuelewa mada mbalimbali zinazotolewa ili waweze kuhudumia wananchi kwa ufasaha.
Aidha Mhe. Msafiri amesema kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba itaanzisha mashamba darasa kwenye Taasisi zote za Serikali ili wakulima waweze kujifunza kilimo bora na chenye tija.
Aidha Ndg Jackson Mahenda Afisa Mradi kutoka shirika lisilo la kiserikali Dalberg amewaomba wataalamu kutoka Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika pamoja na Idara ya Maendeleleo ya Mifugo waandaye vipaumbele vya Halmashauri kulingana na Vipaombele vya Serikali ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi.
Afisa mifugo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg Peter Kasele amesisitiza matumizi ya mizani kwa ajili ya kupimia Mifugo kwenye minada na amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Kwimba kuhakikisha minada yote inamizani na wataalamu wahakikishe wanawafundisha wakulima kuuza mifungo yenye afya bora kwa ajili ya kujipatia kipato kikubwa.
“ Minada yote lazima itumie mizani ili wauzaji wasiibiwe na wanunuzi”
Afisa Mkuu wa Kilimo kutoka Ofisi ya OR-TAMISEMI Ndg Leo Martin amewaambia wataalamu wasifanye kazi kwa kuletewa faili bali waomyeshe ubunifu wa kazi walizozisomea na kuhakikisha wanamsaidia Mkurugenzi Mtendaji kusimamia ukusanyaji mzuri wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
“Tutumie nguvu ya ziada kujenga Mabwawa ya Samaki na tumsaidie Mkurugenzi Mtendaji kuongeza vyanzo vya Mapato kwani hakuna zao lenye mapato mengi kama Ngozi”
Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya OR-TAMISEMI Bibi Upendo Sanga ameiomba Halmashauri kuhakikiksha asilimia za mapato ya Uvuvi, Kilimo pamoja na Mifugo zinarudi kwenye Idara kwa ajili ya Kushughulikia miradi ya maendeleo ya sekta husika.
Mchumi Mkuu kutoka Ofisi y OR-TAMISEMI Bibi Upendo Sanga akichangia mada wakati wa kupitia na kupitisha Mpango kazi kwa mwaka wa fedha 2017/2018
Kwa kuhitimisha Warsha hiyo Bibi Pendo amewashukuru wadau wote wa Kilimo pamoja shirika lisilo la kiserikali Dalberg kwa kusimamia utekelezaji wa Mpango Kazi wa Maendeleo ya Kilimo wilayani kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.