Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari M. Samizi akiwa na kamati ya wataalamu wa Afya ngazi ya Mkoa na Wilaya leo tarehe 06, Oktoba 2021 katika kijiji cha Nyambiti, wametoa elimu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19 kwa Waganga wa Tiba Asili wa Tarafa ya Ibindo Wilaya ya Kwimba.
Waganga hao wamepata nafasi ya kuuliza maswali yaliyokuwa yakiwatatiza kuhusiana na chanjo, ambapo Dakitari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Silas Wambura amewaelezea kuwa chanjo iko salama, haina madhara, amesisitiza kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amejiridhisha kuwa chanjo ni salama ndiyomaana ameileta kwa Wananchi ili wachanjwe kwaajili ya kujikinga na virusi vya corona.
Baada ya Elimu kutolewa Waganga hao wamefanya maamuzi ya kuchanjwa ili kujikinga na kuwakinga wateja wao wanaowafikia kupata huduma katika maeneo yao ya kazi.
l
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.