Mheshimiwa Ester Mahawe Mkuu wa Wilaya ya Mbozi akiwa ameambatana na Kamati ya fedha,uongozi na mipango ya Halmashauri ya Mbozi wamefanya ziara Wilayani Kwimba kujifunza utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa fedha za mapato ya ndani na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Ziara hiyo imefanyika leo Mei 16,2023 ambapo viongozi hao wametembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Budushi Sumve unaotekelezwa kwa millioni 300 fedha za mapato ya ndani. Miradi mingine iliyotembelewa ni ujenzi wa madarasa sita Shule ya Msingi Kabale kwa millioni 121 fedha za mapato ya ndani, mradi wa ujenzi wa uzio wa nyumba ya Mkurugenzi na miradi mingine inayotekelezwa kwa fedha toka Serikali kuu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la utawala na Hospital ya Wilaya.
Mheshimiwa Mahawe ameipongeza Halmashauri ya Kwimba kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi kisha akaahidi kwenda kutumia mbinu walizojifunza Ili kutekeleza miradi yao
"Niwapongeze viongozi wote wa Wilaya ya Kwimba kwasababu mnatekeleza miradi kwa ushirikiano mkubwa sana pia miradi yenu inaonyesha thamani ya fedha, na mbinu yenu tutakwenda kuitumia Wilayani Mbozi Ili tutekeleze miradi mikubwa kwa fedha ya mapato ya ndani" amesema Mahawe
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi Ndugu Abdallah Nandonde ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa utekelezaji wa miradi " ziara yetu imekuwa ya mafanikio sana maana tumejifunza utekelezaji wa miradi pia tumejifunza ukusanyaji wa mapato ya ushiru wa mazao mbinu hizi tukitumia mapato kwenye Halmashauri ya Mbozi yataongezeka"
Waheshimiwa Madiwani kutoka Mbozi wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wengine. Nao wameahidi kwenda kuongeza ushirikiano katika Halmashauri yao.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi kwa fedha za mapato ya ndani Mkurugenzi Mtendaji wa Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri imedhamilia kuwasogezea huduma Wananchi kwa kutumia fedha za mapato ya ndani " tuliona tutenge fedha nyingi zitekeleze mradi mmoja wenye tija, kama ujenzi wa kituo cha Afya"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.