Mradi wa “ Zitambue Haki Zako Mtu Mwenye Ulemavu” unaotekelezwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali The Foundation For Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) –Wilayani Kwimba umetoa mafunzo kwa Wananchi, Walemavu, na Viongozi wa Serikali ngazi ya kijiji ya Ufuatiliaji wa mgawanyo wa Ruzuku Kwa watu wenye Ulemavu Katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali ya Wilaya ya Kwimba.
Mafunzo hayo yalianza tarehe 25 Septemba, 2017 katika kata za Igongwa, Fukalo, Ngudu, Nkalalo na kumalizika katika kata ya Ngula tarehe 29 Septemba, 2017.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Wilayani Kwimba Ndg Nyerere Julias Musa alisema walemavu wana haki ya kuzijua na kuzitambua haki zao, aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo yamewapa fursa ya kupata nguvu ya kudai haki zao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wlemavu Kwimba Ndg Nyerere Julias Musa akitoa Mada wakati wa Mafunzo .
Ndg Nyerere alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kwimba Bibi Pendo Malabeja kwa kupokea andiko lao la Mradi pamoja na kuwapatia ushauri wa hali na mali katika kutekeleza majukumu yao.
Diwani wa Kata ya Nkalalo Mhe. Enos James Ntwale aliiasa jamii kwa kuacha tabia ya kuwaficha watu wenye Ulemavu Majumbani kwani Mradi upo kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatio kama hayo. Aliyasema hayo wakati wa mafunzo katika kijiji cha Mwadubi.
Diwani wa Kata ya Nkalalo Mhe. Enos James Ntwale akiongea na wajumbe wa Mafunzo
Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali MNGON (Umoja wa NGO’S katika mkoa wa Mwanza Ndg Adam Ndokeji aliiomba kamati ya Ufuatiliaji wa Mgawanyo wa Ruzuku kwa Watu Wenye Ulemavu kuhakikisha wanaandika taarifa vizuri zisizopotosha jamii.
Aidha mjumbe wa kamati ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma ujulikanao kwa kiingereza Public Expenditure Tracking System (PETS) Ndg Majingu Bugumba Misongoma ameiomba Serikali kutenga fedha kwa watu wenye ulemavu kupitia bageti kwa ajili ya kupata huduma za Afya kwa sababu kundi hilo linamahitaji maalum.
Ndg Majingu Bugumba Misongoma akiuliza swali wakati wa mafunzo
Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA)-wilayani Kwimba kilianza mwaka 1961 kikiwa na malengo ya kuwaunganisha watu wenye ulemavu wa viungo ili waweze kudai haki zao kwa pamoja na kuleta maendeleo ya chama chao wilayani kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.