Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt. Amon Mkoga ametoa maelezo na taratibu za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27,2024.
Tangazo hilo limetolewa leo 26,Septemba 2024 kwa wadau wa uchaguzi ambapo watu wa makundi mbalimbali wameshiriki mkutano huo ikiwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa vya ACT, CUF, CHADEMA na CCM.
Wadau wengine walioshiriki ni viongozi wa dini, wazee maarufu, watumishi wa umma na wananchi wengine wote waliofika ukumbi wa Halmashauri.
Akitoa tangazo hilo Dkt Mkoga amesema shughuli za Uchaguzi wa Serikali za mitaa zimeanza rasmi ambapo matukio mbalimbali yatafanyika kwa mujibu wa taratibu na sheria za uchaguzi zinazoongoza uchaguzi huo.
Amesisitiza kuzingatia ratiba ya matukio ya uchaguzi ambapo matukio muhimu yameelezwa yakiwemo tarehe 11-20 Oktoba,2024 ni siku za kujiandikisha kwenye daftari la mkazi, tarehe 25 oktoba 2024 ni siku ya kukoma uongozi kwa viongozi walioko madarakani kwa sasa na matukio mengine yote yameelezwa.
Aidha msimamizi wa uchaguzi ametoa rai kwa wananchi wa Kwimba kujitokeza kushiriki matukio yote ya Uchaguzi na kuhakikisha wanashiriki siku ya uchaguzi kuchagua viongozi watakaohamasisha maendeleo ya vijiji vyao.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika tarehe 27,Novemba 2024 ambapo wenyeviti wa vijiji,wajumbe wa Serikali ya kijiji na viongozi wote wa vijiji na vitongoji watachaguliwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.