Msimamizi wa uchaguzi wa majimbo ya Kwimba na Sumve amewatangaza washindi wa ubunge mapema leo tarehe 29/10/2020.
Bib Pendo Anangisye Malabeja msimamizi wa uchaguzi akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi amesema jimbo la Kwimba lilikuwa na watu waliojiandikisha kupiga kura 170671 na waliopiga kura ni 61632.
Wagombea walikuwa wa vyama vitatu
Demokrasia makini Mhe.Kiteja ambaye amepata kura 923
CUF Mhe.Joseph Boniphace ambaye amepata kura 1917 na
CCM Mhe.Shanif Mansoor ambaye amepata kura 57,943
Hivyo Bib. Pendo Malabeja amemtangaza Mhe. Mansoor kuwa mshindi wa ubunge jimbo la Kwimba.
Mhe.Mansoor Mbunge wa Jimbo la Kwimba
Aidha katika jimbo la Sumve msimamizi wa uchaguzi amesema watu wliojiandikisha kupiga kura ni 94029, waliopiga kura ni 39715 na jimbo lilikuwa na wagombea watatu matokeo yalikua kama ifuatavyo
CUF Mhe Joseph Steven amepata kura 722,. CHADEMA Mhe.Sangalali Shija amepata kura 6285 na
CCM Mhe. Emmanuel Kasalali amepata kura 31,373 hivyo msimamizi wa uchaguzi amemtangaza Mhe Kasalali kuwa mshindi wa ubunge jimbo la Sumve.
Mhe. Kasalali Mbunge wa Jimbo la Sumve
Msimamizi wa uchaguzi amewashukuru wananchi wote wa Wilaya ya Kwimba waliojitokeza kupiga kura pia amemshukuru Mungu kwa kuwa uchaguzi umefanyika na kuisha salama kwa majimbo yote mawili.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.