Mwananchi hakikisha umehesabiwa” hii imekuwa kauli mbiu ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi akiwahamasisha watu kuendelea kujiandikisha.
Mapema leo tatehe 26,Agosti 2022 Mhe. Samizi amepita kata ya Mantare, Sumve na Ngudu kukagua zoezi la sensa, hapo ameongea na Wananchi na kuwataka kuhakikisha kila mtu anahesabiwa
“ kila mtu ahakikishe anahesabiwa ili takwimu zipatikane, tusije kuletewa dawa za watu 50 kumbe tuko 100 tukaanza kulalamika dawa hazitoshi,takwimu za sensa zitasaidia kupata huduma kulingana na idadi ya watu” amesema Samizi
Aidha Mkuu huyo amepita kwenye kaya mbalimbali na kuwataka wananchi ambao bado hawajahesabiwa kuwa tayari kutoa ushirikiano pindi watakapofikiwa na makarani wa sensa.
Zoezi la kuhesabu watu na kaya zao linatarajiwa kukamilika tarehe 29,Agosti 2022.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.