Akiongea katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo tarehe 01, Oktoba 2021 kwenye uwanja wa Kwideko Ngudu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza Askofu Charles Sekelwa amesema Wananchi wanapaswa kupuuza maneno yasiyo na tija yanayojaribu kuhafifisha chanjo ya UVIKO-19 ionekane kuwa haifai na haina faida kwa Wananchi.
Askofu huyo amesisitiza kuwa Amani ya waumini inapatika tu pale mtu anapokuwa na Afya iliyo salama hivyo amewaasa Wananchi wote kujitokeza kuchanjwa ili kuwa na uhakika wa kinga dhidi ya UVIKO-19 ugonjwa unaosababisha madhara makubwa pindi unapompata mtu asiye na kinga.
Aidha amesisitiza kuwa Wananchi wasiyajali maneno yanayo enezwa kuwa watu wakichanjwa wanapata madhara yanayopelekea magonjwa mbalimbali, amesisitiza kuwa hayupo kiongozi wa Dini ambaye yuko tayari kuona Waumini wake wanakuwa wagonjwa kutokana na chanjo,
"mimi ni Mchungaji zaidi ya miaka 37 siwezi kuja kudanganya watu kuwa chanjo ina madhara au haina, nimejiridhisha kuwa chanjo ni salama ndipo nikachanjwa na nawahamasisha na nyie mchanjwe, nawasihi ukiona tumeinuka kuja kuwaambia hili ni kwa sababu tuna uchungu na waumini wetu na Nchi yetu pia. Nimesema kama shahidi mtumishi wa Mungu tujiepushe na propaganda zisizo za kweli". amesema Askofu Sekelwa
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa Dini mbalimbali akiwemo Sheikh Mohamedi Moledina ambaye amewataka wananchi kuzitumia Dini vizuri ili ziweze kuleta manufaa kwa Jamii, amesisitiza kuwa Dini zikitumika vizuri zinaweza kuunganisha watu lakini zikitumika vibaya zinatenganisha watu na kuleta madhara makubwa katika Jamii.
Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robart Gabriel amewashauri Wananchi kuchanjwa chanjo ya UVIKO-19 ili kujihakikishia kinga dhidi ya virusi vya corona na kuona umuhimu wa kuwa na Afya njema ili kuendelea kuzitunza familia zao na kuendelea kulitumikia Taifa. Kutokana na Elimu hiyo iliyotolewa na viongozi Wananchi wamejitokeza kuchanjwa ambapo zoezi la Chanjo limefanyika hapo hapo katika uwanja wa Kwideko.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.