Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Taifa Ndugu Mary Pius Chatanda amewataka wafanya biashara kuzingatia sheria na taratibu za ukusanyaji mapato
" wafanya biashara nawafahamu acheni ujanjaujanja acheni kusafirisha mazao kidogokidogo kwenye bajaji pelekeni magari yenu makubwa mnakochukulia mazao ili muepuke kutozwa ushuru mara mbili"
Ameyasema hayo leo kwenye mkutano alioufanya kata ya Hungumalwa na Ngudu baada ya wananchi wa kata hizo kulalamika kuhusu kutozwa ushuru wanapobeba mazao kwenye bajaji.
Aidha Chatanda amewashauri wananchi kuzingatia taratibu za serikali ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria za kusafirisha mazao
" niwashauri mzingatie sheria ukitaka kusafirisha mazao kutoka shambani kwenda nyumbani hakikisha unapata barua kutoka kwa mtendaji wa kijiji ili usitozwe ushuru"
" hakuna Halmashauri bila mapato, ushuru huo unaokusanywa ndio unarudi kutekeleza miradi mbalimbali kwahiyo niwashauri lipeni ushuru kwa maendeleo ya Kwimba na Taifa kwa ujumla
Awali Mwenyekiti huyo akikagua mradi wa Kituo cha Afya hungumalwa amepongeza viongozi waliosimamia utekelezaji wa mradi huo na ameahidi kufuatilia vifaa tiba ambavyo bado havijaletwa hali inayopelekea baadhi ya hiduma kutopatikana kituoni hapo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Ndug Denis Kabogo akijibu hoja ya ushuru amesema kuwa Halmashauri imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa ushuru bila shuruti huku akisisitiza kuwa ushuru unalipwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za ushuru wa mazao.
Aidha Chatanda ametumia ziara hiyo kuhamasisha wananchi kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura pia amewatangazia wanawake vijana na watu wenye ulemavu kuchukua mikopo ya Halmashauri mikopo iliyokuwa imesitishwa sasa imeshaanza kutolewa
" kachukueni mikopo ambayo haina riba mikopo ya rais Samia haina riba achaneni na mikopo umiza, kausha damu na mikopo mingine inayowatesa kurejesha" amesema chatanda.
Wananchi walioshiriki mikutano hiyo wamemshukuru kiongozi huyo kwani wamepata wasaa wa kuuliza hoja mbalimbali na zimepatiwa majibu
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.