Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bara Ndugu Christina Mndeme aipongeza Kwimba kwa kupata miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Hungumalwa, ameyasema hayo leo tarehe 11,Agosti 2022 katika Kituo cha Afya Hungumalwa wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho ambapo Kata ya Hungumalwa ilipokea milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya.
“ tunaposema Mama Samia anaupiga mwingi hii ndiyo maana yake tarifa yenu imesema Kwimba mmepokea bilioni 28 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ndiyo maana ukienda kweye sekta ya Afya unamkuta mama Samia ,barabara unamkuta,maji yupo,Elimu, na miradi mingine hongereni sana Kwimba”amesema Mndeme
Kiongozi huyo amesisitiza mwezi wa tisa kituo cha Afya Hungumalwa kiwe kimekamilika na kuanza kutoa huduma, ili lengo la kutoa huduma kwa Wananchi likamilike.Aidha amewaelekeza Madaktari na wauguzi kuongeza uboreshaji wa huduma za Afya ikiwa na lengo la kupunguza vifo vinavyowezekana kuepukika
“ niwaombe sana wauguzi na madaktari mboreshe huduma za Afya, mgonjwa anapokuja hospitali apate matumaini ya kuishi siyo wagonjwa wanafika hospitali wanakosa matumaini, toeni huduma bora” amesema Mndeme
Akiongea na viongozi na Wananchama wa Chama Cha Mapinduzi katika Tawi la Malya na Ngudu, Mndeme amewataka viongozi wa Chama na Serikali kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ili adhima yake ya kufikisha maendeleo kwa Wananchi itimie.
Aidha kiongozi huyo amesisitiza upandaji wa miti inayovumilia ukame na hali ya hewa ya Kwimba, miti itakayosaidia kuzuia upepo mkali unaoweza kuezua mapaa ya majengo, lakini miti itaweza kuyafanya mazingira yawe na muonekano mzuri.
Akihitimisha hotuba yake ametoa Elimu ya Sensa, amewashauti wananchi wote kuwa tayari kuhesabiwa ifikapo tarehe 23,Agosti 2022 .
Naye Mkurugenzi wa Halmashairi akisoma taarifa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ikiwemo miradi ya Afya, Elimu, maji, barabara, umemena mingine
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.