Naibu waziri wa Ardhi Mhe.Angelina Mabula amefanya ziara ya kikazi Wilayani Kwimba kufuatilia maagizo aliyoyatoa kama yanafanyiwa kazi,kuhamasisha watumishi wa Idara ya Ardhi kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa urasimishaji wa Ardhi na kuhamasisha Idara ya Ardhi juu ya ukusanyaji wa mapato yanayotokana na Ardhi.
Katika ziara hiyo Mhe.Angelina ametoa hati 13 kwa wamiliki ambao wamefanya umirikishwaji wa Ardhi akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri Bib.Pendo Malabeja ambaye amepokea hati ya eneo la Halmashauri.
Aidha Mhe.Angelina ameitaka idara ya Ardhi kuongeza malengo ya idadi ya utoaji wa Hati kwa mwaka na amesisitiza elimu itolewe ili wananchi wajue faida za kumilikishwa ardhi,ili wajitokeze kwa wingi kurasimisha ardhi zao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.