" ninaimani kubwa sana na Walimu wote" haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija katika kikao kazi cha Walimu wa Tarafa ya Ngula kilichofayika April 13,2023 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Sumve
"ninaimani na walimu wote kwasababu sisi wote ni zao la walimu bila ninyi hakuna taaluma, kwahiyo tunathamini kazi kubwa ambayo mnaifanya na kila mmoja kwa nafasi yake endeleeni kutekeleza wajibu wenu" amesema Ludigija
Walimu hao wametakiwa kuendelea kufundisha kwa kuzingatia taratibu,sheria na kanuni zinazoongoza kazi hiyo,pia wameshauriwa kuitendea haki kazi yao kwa kuhakikisha wanaongeza ufaulu wa wanafunzi.
Mkuu huyo amesisitiza kuwa kazi ya ualimu ni kazi ya heshima hivyo Walimu waendelee kuiheshimisha kazi hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia haiba ya mavazi na tabia njema katika jamii.
Katika kikao hicho ameshiriki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi.Happiness Msanga ambaye amewataka Walimu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za utumishi
"zingatieni miiko ya utumishi na uwajibikaji kwa mwalimu unaonekana sana kwasababu mwalimu anapimwa kwa kuangalia mwanafunzi anayemfundisha mtoto akishida hapo mwalimu anaonekana anafanya kazi kwihiyo fanyeni kazi, pia acheni utoro " amesema Msanga
Walimu hao wamefurahia kushiriki kikao kazi hicho kwani wamepata nafasi ya kuwasilisha kero zao na zikatolewa majibu,pia wameshauri vikao hivyo vifanyike marakwamara ili visaidie kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utumishi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.