Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Emmanuel Katemi amepokea computa 10 kutoka Taasisi ya fedha NMB kwaajili ya shule za Sekondari tano zenye kidato cha tano na sita.
Vifaa hivyo vimepokelewa leo Agost 7,2024 kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri " nitumie nafasi hii kuishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kushiriki uboreshaji wa elimu kwa kutoa vifaa hivi vya TEHAMA, vitasaidia sana katika ufundishaji na ujifunzaji" Katemi
Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa NMB Ngudu Hassan amesema ni utaratibu wa benki hiyo kutoa misaada ya vifaa katika taasisi za elimu na Afya ikiwa na lengo la kurudisha mchango kwa jamii
Nao walimu waliopokea vifaa hivyo wameishukuru NMB kwa kujali na kushiriki uboreshaji wa elimu pia wameiomba taasisi hiyo kuendelea kutoa vifaa mbalimbali
" nipende kuishukuru NMB kwa kuona umuhimu wa kuleta vifaa hivi tunaamini kupitia vifaa hivi elimu itaboreshwa zaidi" amesema Mwalimu Komenikesha
Aidha Afisa Elimu amesema shule hizo zilizopewa vifaa zimefanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita hivyo kuongezeka kwa vifaa hivyo vya TEHAMA kutachangia ufaulu kuongezeka zaidi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.