Mhe. Aggrey Mwanri akiendelea kutoa elimu ya kilimo bora cha Pamba katika vijiji vya Nyagh'onge, Sangu, Bupamwa, Kikubiji na Shirima leo tarehe 10/11/2921 amewaasa Wakulima kutochafua Pamba wakati wa mavuno kwa lengo la kuongeza uzito.
Mhe. Mwanri amesema kuwa Wakulima wengi wanapunguza ubora wa pamba kwa kuweka vitu mbalimbali vinavyopelekea pamba hiyo kushuka thamani.
" mnaweka mchanga, kokoto, mafuta ya kenge na hiyo haitoshi mnapiga sindano yaani kunyunyiza maji ili iwe nzito, kufanya hivyo mnachafua Pamba na hii inakufanya ulipwe robo ya bei ya pamba au isinunuliwe kabisa, nani ananunua hiyo takataka? Wananchi acheni mchezo huo" amesema Mwanri
Katika mafunzo hayo Wananchi wamepata nafasi ya kujifunza kupalilia Pamba kwa kutumia Jembe maalum la kupalilia linalokokotwa na Wanyama kazi yaani ng'ombe au punda, ambapo Mkulima akitumia jembe hilo anauwezo wa kupalilia ekari moja kwa masaa mawili tu.
Afisa Kilimo kutoka bodi ya Pamba Ndug. Renatus Luneja amewashauri wakulima kutumia jembe hilo ambalo litawarahisishia kazi ya upaliliaji na hivyo kuwaharakishia kazi za kilimo . Jembe hilo linapatikana kwa bei ya shilingi 250,000 ambapo mkulima atatoa Laki moja ili apewe jembe hilo kisha fedha nyingine atalipa baada ya mavuno, utaratibu wa kupata majembe hayo utafanyika katika Ofisi za vijiji.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.